Klabu ya Yanga sc imevunja mkataba na mchezaji wake Carlos Carlinhos baada ya makubaliano ya pande mbili kuvunja mkataba huo uliokua umebakiza mwaka mmoja kumalizika.
Inasemekana hii mara ya tatu kwa kiungo huyo kuwasilisha maombi ya kuvunja mkataba na mabingwa hao mara 27 wa ligi kuu nchini lakini uongozi wa klabu hiyo ulifanikiwa kutatua migogoro hiyona kuhakikisha mchezaji huyo anakua na amani klabuni hapo.
Hata hivyo katika makubaliano ya kuvunja mkataba huo klabu ya Yanga sc imeweka vipengele kadhaa ikiwemo kulipwa kiasi cha dola laki mbili endapo atapata timu ya ndani ya nchi na pia mchezaji atalazimika kulipa asilimia 75 ya dau la usajili endapo atapata timu nje ya Tanzania.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.