Klabu ya Yanga sc imetangaza tenda kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Hosteli pamoja na uwanja wa mazoezi Kigamboni jijini Dar es salaam.
Tenda imetangazwa kupitia mitandao ya kijamii ya klabu hiyo ambapo wahusika wa masuala ya ujenzi wanatakiwa kutuma maombi.
Klabu hiyo mnamo mwaka huu ilikabidhiwa viwanja na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam aliyepita Paulo Makonda.