Klabu ya Yanga sc imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 mchezo wa kirafiki dhidi ya Mlandege Fc kutoka visiwani Zanzibar uliofanyika katika uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es salaam.
Yanga iliyochezesha vikosi viwili huku kile cha mastaa kikicheza dakika 45 za kipindi cha pili ilipata mabao yake kupitia kwa Waziri Junior kwa penati kipindi cha kwanza baada ya beki wa Mlandege kuunawa mpira ndani ya 18 wakati akijaribu kuokoa pasi ya Haruna Niyonzima.
Mukoko Tonombe aliipatia Yanga sc bao la pili dakika ya 59 kwa shuti kali baada ya kupokea pasi ya Yacouba Sogne na mpaka dakika ya 90 matokeo yalisalia hivyo hivyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Yanga itasafiri kesho kuifuata Kagera Sugar siku ya Jumamosi mchezo utakaofanyika katika uwanja wa Kaitaba mkoani humo.