Msafara wa watu 38 wa timu ya Yanga sc umeondoka mchana wa leo kuelekea jijini Mbeya katika mchezo waligi kuu dhidi ya Mbeya city utakaofanyika siku ya jumammosi katika uwanja wa Sokoine.
Msafara huo unaojumuisha wachezaji 24 huku idadi ya viongozi na benchi la ufundi ikiwa 14 umeondoka leo kwa ndege ya shirika la ndege la Air Tanzania kuelekea kuivaa timu hiyo katika awamu ya pili ya ligi kuu Tanzania huku kumbukumbu katika mchezo wa awali uliofanyika jijini Dar es salaam Yanga sc iliibuka na ushindi wa bao 1-0.