Klabu ya soka ya Yanga imeanza vyema harakati zake za kutwaa ubingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara kwa ushindi wa goli 1-0 ugenini dhidi ya wenyeji Kagera Sugar katika mchezo wao wa kwanza wa ligi hiyyo.
Katika mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba,Yanga ilijipatia bao lake pekee dakika ya 24 kupitia kwa nahodha wao wa leo Feisal Salum kwa shuti kali la chini akimalizia mpia uliookolewa na golikipa wa Kager Ramadhan Chalamanda.
Mabingwa hao wa kihistoria waliitwala mechi hiyo kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha kwanza kwa pasi nyingi fupifupi na endapo wangezitumia vyema nafasi walizotengeneza basi wangeweza kufunga hata magoli matatu katika kipindi hicho.
Kagera Sugar walicheza vizuri kipindi cha pili lakini shukrani kwa uimara wa mabeki Yanick Bangala na Dickson Job kambao ambao walikuwa imara kulinda lango la wanachi.
Yanga iliwakosa wachezaji wake nahodha Bakari Mwamnyeto aliyepata majeraha na Mukoko Tonombe anayetumikia adhabu ya michezo mitatu baada ya kupata kadi nyekundu kwenye fainali ya kombe la shirikisho la Azam.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Wanchi hao wanashika nafasi ya nne katika ligi hiyo wakiwa na alama tatu baada ya mchezo mmoja,msimamo kamili wa ligi kuu soka Tanzania Bara baada ya michezo ya kwanza ni kama ifuatavyo;