Home Soka Yanga yanasa straika Mbeya

Yanga yanasa straika Mbeya

by Sports Leo
0 comments

Mabingwa wa kihistoria nchini Yanga sc imefanikiwa kuinasa saini ya mshambuliaji wa Mbeya Kwanza Crispin Ngushi na kumtambulisha rasmi usiku wa kuamkia leo ndani ya makao makuu ya klabu hiyo Jangwani.

Mchezaji huyo amekuwa akiwafanya vizuri msimu huu tangu ajiunge na Mbeya Kwanza akitokea huko Malawi alipokuwa akicheza soka la kulipwa katika nchi hiyo.

Usajili huu unatajwa kuwa ni kama ujasusi umefanyika kumpora straika huyo kutoka kwenye rada za mpinzani wao wa jadi Simba waliokuwa katika hatua za mwisho kumhamishia katika viunga vya mitaa ya Msimbazi,lakini ni kazi kubwa kutoka kwa mjumbe wa kamati ya usajili wa Yanga Injinia Hersi Said aliyefanya umafia na kumshawishi kutua Jangwani kutokana na nguvu ya pesa.

banner

Ngushi ana kazi kubwa kumshawishi kocha Nasreedin Nabi kumpatia nafasi ya kucheza ndani ya timu hiyo kwenye idara ya ushambuliaji ukizingatia uwezo mzuri unaooneshwa na wanaocheza kwasasa wakiongozwa na Fiston Mayele.

Hata hivyo bado ni suala la kusubiria ni kwa kiasi gani ataendana na mahitaji ya mwalimu na timu kwa ujumla kwani ana uwezo mzuri wa kufunga na kutengeneza mabao.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited