Home Soka Ziyech Mikononi Mwa Lampard

Ziyech Mikononi Mwa Lampard

by Sports Leo
0 comments

Kocha wa klabu ya Ajax Amsterdam, Eric Tel Hag, amethibitisha kuwa kiungo wake, Hakim Ziyech, atajiunga na klabu ya Chelsea mwishoni mwa msimu baada ya pande mbili kufikia makubaliano.

Ajax na Chelsea wamefikia makubaliano ya ada ya kiasi cha paundi milioni 38, ili kufanikisha dili hilo la kiungo huyo mshambuliaji raia wa morocco

Ziyech ambaye ni kiungo mshambuliaji asilia akiwa na uwezo wa kucheza kulia na kushoto aliisaidia Ajax kutinga hatua ya nusu fainali ya Uefa Champions League msimu uliopita huku akicheza mechi 49 na kufunga mabao 21 na kuasisti mabao 24 katika michuano yote.

banner

Licha ya kusaidia Ajax kutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini Uholanzi pia ameifungia timu hiyo mabao 48 na kusaidia upatikanaji wa mabao 82 katika mechi 160 alizoichezea timu hiyo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited