Home Makala Ndemla Aikoa Mtibwa Sugar

Ndemla Aikoa Mtibwa Sugar

by Sports Leo
0 comments

Kiungo wa klabu ya Mtibwa Sugar Said Ndemla ameikoa klabu yake kukosa alama tatu baada ya kufanikiwa kufunga bao katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Mbeya City katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Manungu Stadium mkoani Morogoro.

Ndemla alifunga bao hilo dakika ya 15 ya mchezo kwa shuti kali baada ya kupokea pasi nje kidogo ya eneo la hatari la mita 18 na kufumua shuti lililomshinda golikipa Deo ‘Dida’ Munishi wa Mbeya City.

Kutokana na ushindi huo sasa mtibwa imefikisha jumla ya alama 27 huku ikiwa katika nafasi ya nane ya ligi kuu nchini na Mbeya City ikiwa katika nafasi ya saba na alama 28.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited