Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imepoteza mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan) baada ya kukubali kipigo cha 1-0 kutoka kwa Uganda katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.
Stars ilijitahidi kucheza kwa kupanga mashambulizi ya uhakika lakini uimara wa safu ya ulinzi ya Uganda ukawa kikwazo kupata bao hali iliyodumu mpaka mapumziko ya kipindi cha kwanza bila kupata bao.
Zikiwa zimesalia dakika tatu mchezo kukamilika, Uganda waliweza kupachika bao kupitia kwa Travis Mutyaba dakika ya 87 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa bao ambalo lilianzia upande wa kushoto baada ya Mohamed Hussein kushindwa kuokoa mpira na kumkuta mfungaji.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kutokana na matokeo hayo Taifa Stars inakabiliwa na mtihani mzito wa kusaka ushindi wakati wa mchezo wa marudiano nchini Uganda ambapo haitakua na matokeo mengine yenye nafuu zaidi ya ushindi wa kuanzia mabao mawili huku wakihakikisha wenyeji hawapati bao.