Home Soka Staa Real Madrid Ala Bata Tz

Staa Real Madrid Ala Bata Tz

by Dennis Msotwa
0 comments

Mchezaji wa Real Madrid ya hispania Theo Hernandez ameonekana nchini Tanzania katika mbuga ya Serengeti akiwa na mrembo ambaye inasemekana ni mpenzi wake.Beki huyo Raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 21 ametembelea nchini kimyakimya katika mapumziko ya mwisho wa msimu wa ligi mbalimbali duniani ambapo mastaa mbalimbali hutembelea sehemu tofautitofauti kupumzika na kufurahia na wenza wao.

Theo ameonekana yupo nchini baada ya kuposti picha katika mtandao wa instagram akila bata na mpenzi wake huyo.Katika picha hizo tatu,moja alionekana akiwa amesimama mbele ya  bwawa la kuogelea na mpenzi wake Adriana Pozueco huku picha mbili akiwa ndani ya gari la kutembelea watalii mbugani.

banner

Theo ambaye analipwa mshahara wa yuro milioni 2.7 huku akiwa na utajiri wa dola milioni 9 alijiunga na Real madrid Julai 5,2017,anacheza nafasi ya beki wa kushoto ni mchezaji wa wababe hao wa hispania ambao walimsajili japo hivi sasa msimu ulioisha aliitumikia timu ya Real Sociaded baada ya kutolewa kwa mkopo na mabingwa hao wenye historia ya kuchukua taji la klabu bingwa ulaya(Uefa) mara tatu mfululizo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited