Home Makala Simba sc Kiboko Kimataifa

Simba sc Kiboko Kimataifa

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba sc imeonyesha ukubwa wake katika michuano ya kimataifa baada ya kufanikiwa kuifunga klabu ya Premero de Augosto ya Angola kwa mabao 3-1 katika mchezo wa ligi ya mabingwa hatua ya pili uliofanyika nchini Angola siku ya jumapili Oktoba 16 katika uwanja wa Estadio 11 de Novembro.

Simba sc ikiwa ugenini ilianza kupata bao la mapema kupitia kwa Cletous Chama dakika ya 9 ya mchezo akipokea pasi ya mpenyezo kutoka kwa Augustine Okra bao ambalo lilidumu mpaka mapumziko ambapo kipindi cha pili Simba sc ilipata bao la pili likifunga na Israel Mwenda aliyepokea pasi ya Chama dakika ya 63 na baadae dakika ya 75 Moses Phiri alifunga bao la tatu lililomaliza kabisa nguvu ya waangola.

Dakika mbili baada ya kuingia kwa bao hilo waaangola nao walicharuka na kupata penati baada ya beki Kennedy Juma kuunawa mpira katika eneo la hatari na hatimaye Dago Tshibamba Samu kufunga bao la kufutia machozi kwa wenyeji.

banner

De Augosto watakua na kibarua kigumu cha kusawazisha mlima mkubwa watakapokuja nchini kuwavaa Simba sc siku ya Jumamosi ya Oktoba 15 katika mchezo ambao utafanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam ambapo mshindi atakwenda katika hatua ya makundi ya kombe hilo kubwa barani Afrika kwa ngazi ya vilabu.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited