Mastaa kadhaa wa klabu ya Simba sc watakosekana katika mchezo dhidi ya Azam Fc kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo majeraha na kuwa na kadi za njano ambapo mastaa hao ni Mzamiru Yassin,Sadio Kanoute,Jimson Mwinuke na Israel Patrick.
Kwa mujibu wa maofisa wa Simba sc Sadio Kanoute yeye anaugua tonsils (mafindofindo), Israel Patrick amepata majeraha katika mchezo uliopita dhidi ya Yanga. ambao walitoka sare ya 1-1 huku wengine kama Jimmyson Mwanuke ambaye bado anaendelea kuuguza majeraha na Mzamiru Yassin anayetumikia adhabu ya kadi tatu za njano.
Simba sc itavaana na Azam Fc katika mchezo mkali wa leo jioni huku wakilazimika kutafuta ushindi ili kurudi kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ambapo jana Yanga sc walipanda juu ya msimamo baada ya kuifunga Kmc kwa bao 1-0 lililofungwa na Feisal Salum.
Azam Fc wanatarajiwa kutoa upinzani mkali baada ya hivi karibuni kumtimua mwalimu Dennis Lavigne na kuwakabidhi majukumu Kally Ongala na Aggrey Morris kuongoza jahazi la timu hiyo ambayo ipo katika nafasi ya tisa ya msimamo wa ligi kuu nchini ikiwa na alama 11 katika mchezo saba ambapo mchezo wa mwisho ilipoteza kwa 2-1 dhidi ya Kmc.