Jean Baleke ametambulishwa kuwa mchezaji mpya wa klabu ya Simba sc kwa mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja baada ya timu hizo mbili kufikia makubaliano huku kukiwa na kipengele cha kuongeza zaidi muda huo kwa mchezaji huyo.
Baleke mwenye miaka 21 amejiunga na klabu ya Simba sc akitokea nchini Lebanon alipokua anacheza katika klabu ya Nejmeh SC ya nchini humo na baada ya mkopo huyo kuisha alilazimika kurudi Tp Mazembe na kisha akapata dili hilo la kujiunga na Simba sc.
Baleke aliwahi kuwa mfungaji bora wa ligi kuu nchini Congo msimu wa 2020/2021 akiwa na timu ya JS Kinshasa alipofunga jumla ya magoli 14 na akafanikiwa kusajiliwa na Tp Mazembe msimu uliofuatia lakini kiwango chake hakikuwaridhisha mabosi hao na kuamua kumtoa kwa mkopo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Simba sc imefanikiwa kumsajili staa huyo kuja kuongeza nguvu eneo la ushambuliaji lililokua chini ya Moses Phiri na Cletous Chama ambapo sasa kutakua na machaguo mbalimbali eneo hilo la ushambuliaji.