Home Makala Mastaa Simba sc Wadai Posho

Mastaa Simba sc Wadai Posho

by Sports Leo
0 comments

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba Sc Ahmed Ally Amekiri wachezaji wa Timu hiyo kudai bonasi za michezo mbalimbali ambayo hupatiwa kwa mujibu wa utaratibu wa klabu hiyo.

Ahmed alisema kwamba imekua ni kawaida kwa klabu hiyo kutoa bonasi ya kiasi cha fedha kwa ajili ya mastaa wa klabu hiyo kwa mechi wanazoshinda na kutoa sare huku akisisitiza kuwa kutolipwa kwa fedha hizo ni hali kawaida kwa taasisi kudaiwa ambapo wakipata basi hulipa madeni hayo.

“Ni kweli wachezaji wanadai Bonasi zao za mechi kadhaa, Kuna wakati taasisi inakuwa na fedha inalipa madeni yote Kuna wakati haina fedha inalimbikiza madeni Mzigo ukipatikana watu wanalipwa”

banner

Ahmed Ally Ameongeza kuwa ni kawaida kwenye taasisi ya biashara watu kucheleweshewa miezi miwili au mitatu lakini hiyo sio sababu ya kufungwa na Azam FC katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la shirikisho la Azam Sports.

“wametufunga mara mbili wametuzidi ubora”Alimalizia kusema Ahmed ambaye ni meneja habari wa kisasa na kijana katika klabu hiyo yenye makazi yake mitaa ya msimbazi kariakoo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited