Klabu ya Simba sc imetangaza kumrejesha beki wa pembeni David Kameta maarufu kama Duchu ambaye alikua kwa mkopo katika klabu ya Mtibwa Sugar ambapo amesaini mkataba wa miaka mitatu kuendelea kusalia klabuni hapo.
Awali Duchu alisajiliwa na Simba sc akitokea Lipuli Fc lakini kutokana na changamoto ya namba alitolewa kwa mkopo katika klabu mbali mbali zikiwemo Geita Gold Fc na baadae akajiunga na Mtibwa Sugar ya manungu morogoro.
Simba sc imelazimika kumsajili beki huyo kuja kusaidiana na Shomari Kapombe upande wa kulia huku ikihamishia mlinzi wake Israel Mwenda upande wa kushoto kusaidiana na Mohamed Hussein hasa baada ya kumkosa beki waliyepanga kumsajili Yahaya Mbegu ambaye amejiunga na Singida Fountain Gate Fc.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.