Home Makala Skudu ni Mwananchi

Skudu ni Mwananchi

by Dennis Msotwa
0 comments

Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Mahlatse Skudu Makudubela kuwa mchezaji wao baada ya kukamilisha usajili wa kujiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Skudu ambaye alikua akiitumikia klabu ya Marumo Gallants ambayo imeshuka daraja licha ya kufanya vizuri katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Mchezaji huyo ndie ambaye alikua akisubiriwa na mashabiki wengi wa soka nchini baada ya mkuu wa idara ya habari ya klabu hiyo kumpigia kampeni kubwa akitaja kama namba sita hatari ambapo atarithi jezi iliyoachwa na Feisal Salum aliyejiunga na Azam Fc.

banner

Skudu anatajwa kama winga mwenye kasi kubwa pamoja na kujua chenga za maudhi huku pia akisifika kwa mpira wa burudani japo kwa takwimu za ligi kuu ya Afrika kusini msimu uliopita zinaonyeshwa kwamba katika michezo 22 amefunga mabao mawili na kutoa asisti mbili pekee.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited