Droo ya makundi ya kombe la klabu bingwa barani Afrika imefanyika siku ya ijumaa ambapo jumla ya makundi manne yametangazwa huku klabu ya Yanga sc ikiangukia katika kundi D ambalo ndio linasadikika kuwa kundi gumu zaidi katika makundi hayo manne.
Makundi hayo kama yanavyoonekana pichani yamezua gumzo hasa nchini Tanzania ambapo klabu ya Simba sc imeonekana kama imepata kundi laini zaidi tofauti na wenzao Yanga sc.
Mechi za hatua ya makundi zinatarajiwa kuanza mwezi Novemba mwishoni ambapo klabu ya Yanga sc itaanzia ugenini nchini Algeria kuwavaa CR Belouzdad huku Simba sc ikianzia nchini kuwavaa Asec Mimosas ya nchini Ivory Coast.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.