Staa wa klabu ya Singida Fountain Gate FrancyKazadi amekalia kuti kavu klabuni humo kutokana na kiwango chake kushindwa kuwashawishi mabosi wa klabu hiyo tangu msimu huu uanze ambapo amekosa namba mbele ya Elvis Rupia.
Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema wapo mastaa ambao wanafanyiwa tathimini kuanzia sasa na kama benchi la ufundi halitaridhika na viwango vyao watapewa mkono wa kwaheri dirisha dogo litakapofunguliwa akiwemo staa huyo ambaye alitamba katika dirisha dogo la msimu uliopita hasa katika michuano ya kombe la mapinduzi visiwani Zanzibar.
“Ni kweli tumeanza kufanya tathimini ya kila mchezaji lakini tunaangazia sana kwa wale wa kigeni kwa sababu ndio ambao tunatumia fedha nyingi kuwalipia, Kazadi ni miongoni mwao ila ni mapema na lolote linawezekana.”Alisema bosi mmoja wa klabu hiyo
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Mpaka sasa klabu hiyo ipo katika nafasi ya tisa ya msimamo wa ligi kuu ya Nbc ikiwa na alama tano tu katika michezo mitano ya ligi kuu huku tayari ikiwa imetolewa katika michuano ya kimataifa baada ya kufungwa na Future Fc kwa jumla ya mabao 4-2 na kushindwa kufuzu hatua makundi ya kombe la shirikisho.