Klabu ya Yanga sc ipo mbioni kukamilisha usajili wa mchezaji Glody Kilangalanga ambaye anaitumia klabu ya Bisha Fc inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Saudi Arabia baada ya kutorodhika na washambuliaji waliopo klabuni hapo.
Mpaka sasa jitihada zinafanyika kwa mabosi wa Yanga sc kumpata mshambuliaji huyo ama kwa kumsajili moja kwa moja na ikishindikana basi apatikane kwa mkopo kuja kuchukua nafasi ya Hafiz Konkoni ambaye mabosi hao hawajaridhishwa na uwezo wake wa kufumania nyavu mpaka sasa.
Bisha Fc bado ina mkataba na straika huyo ambaye ilimsajili kutoka Cs Cheba ya nchini Tunisia na mpaka sasa ndiyo inaleta ugumu katika kuinasa saini ya mshambuliaji huyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Yanga sc awali ilikua na mpango wa kusajili Karamoko Sankara wa Asec Mimosa,Saimon Msuva ama Ranga Chivaviro sajili ambazo zilikwama kutokana na sababu mbalimbali.