Home Soka Chirwa Ajisalimisha Azam

Chirwa Ajisalimisha Azam

by Sports Leo
0 comments

Mshambualiaji wa Azam fc Obrey Cholla Chirwa amejisalimisha klabuni hapo na kusaini mkataba mpya wa mwaka mmoja baada ya kuwazungusha viongozi wa klabu hiyo kwa muda mrefu bila sababu zisizoeleweka.

Mchezaji huyo wa zamani wa Yanga sc na Platnum Fc ya Zimbabwe aliitwa mara kadhaa na viongozi wa klabu hiyo inayoongozwa na Mtendaji mkuu Abdulkarim Amin ”Popat” ambaye aliamua timu hiyo kuachana na staa huyo na kutoa orodha yenye majina ya mastaa kibao ambao timu hiyo imeachana nao na jina la mzambia huyo kuwamo.

Inaripotiwa baada ya timu hiyo kufikia uamuzi huo,staa huyo alishtuka na kuamua kuwafuata viongozi hao na kusaini mkataba mpya wa mwaka mmoja fasta baada ya kocha mpya wa timu hiyo Ettiene Ndayiragije kupitisha suala hilo na kuifanya timu hiyo kubaki na nafasi mbili za usajili kati ya nne maana tayari imewasajili Idd Seleman Naddo na Chirwa.

banner

Azam inajiandaa na msimu ujao wa ligi kuu bara ambapo pia itashiriki michuano ya shirikisho barani Afrika baada ya kupata tiketi kufuatia idadi ya timu za Tanzania kuongezeka kutoka mbili hadi nne japo pia ilikua na uhakika wa kushiriki baada ya kuwa bingwa wa kombe la shirikisho.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited