Home Soka Kivumbi Nusu Fainali Afcon

Kivumbi Nusu Fainali Afcon

by Sports Leo
0 comments

Michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon 2023) sasa imeingia hatua ya nusu fainali ambapo timu nne za Congo Drc,Nigeria,Ivory Coast na Afrika kusini watamenyana kuwania nafasi ya kuingia fainali ya michuano hiyo inayoendelea nchini Ivory Coast.

Nigeria walifuzu nusu fainali wakiifunga Angola 1-0 bao la dakika ya 41 la Ademola Lookman huku Congo Drc wakiifunga 3-1 Guinnea mabao ya Chancel Mbemba dakika ya 31,Yoanne Wissa dakika ya 65 na Arthur Masuaku dakika ya 81 ya mchezo na kujihakikishia tiketi ya nusu fainali.

Wenyeji Ivory Coast waliifunga Mali 2-1 mabao ya Simon Adingra dakika ya 90 na Oumar Diakite dakika ya 120+2 na kuwaacha Mali na vilio baada ya kuukamata mchezo dakika zote tisini huku Afrika ya Kusini wakiifunga Cape Verde kwa penati 2-1 ambapo kipa Ronwel Williams aliibuka shujaa akidaka penati nne.

banner

Michuano hiyo itaendelea siku ya Jumatano ambapo Nigeria watavaana na Afrika kusini huku wenyeji Ivory Coast wakivaana na Congo Drc kukata tiketi ya kuingia fainali.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited