Home Soka Mwamnyeto Uhakika Yanga Sc

Mwamnyeto Uhakika Yanga Sc

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kumuongeza mkataba wa miaka miwili beki na nahidha wake Bakari Mwamnyeto baada ya kufikia makubaliano na uongozi wa staa huyo huku kukiwa na maboresho makubwa ya fedha ya kusainia mkataba huo.

Mabosi wa Yanga sc wanamuona beki huyo akiwa ni sehemu ya mpango wa muda mrefu wa kikosi hicho sambamba na mabeki wenzake Ibrahim Bacca na Dickson Job hivyo kumuacha ni sawa na kuachia silaha ya ushindi vitani.

banner

Tayari mkataba huo umeshasainiwa na sasa kilichobaki ni kutambulishwa pekee huku tetesi za kuwa anatakiwa na klabu ya Simba sc zikiwa zimezimwa tayari kutokana na dili hilo kukamilika.

Mwamnyeto kwa miaka mitatu amekua ni nahodha mwenye mafanikio zaidi nchini akibeba mataji ya ligi kuu na kombe la shirikisho mara tatu huku akipata mafanikio zaidi tangu alipojiunga na timu hiyo akitokea Coastal Union mwaka  2020.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited