Mshambuliaji Erick Okutu raia wa Ghana amejiunga na klabu ya Pamba jiji akitokea Tabora United kwa mkataba wa mwaka mmoja baada ya kumaliza mkataba na klabu yake hiyo ya zamani iliyompokea nchini msimu uliopita.
Erick alifanikiwa kufunga mabao 7 msimu uliopita akiwa chini ya kocha Goran Kopunovic ambaye kwa sasa ni kocha wa Pamba Jiji baada ya kuondoka Tabora United akijiuzuru nafasi yake ya ukocha mkuu kutokana na masuala ya malipo kutokua sawa.
Tayari kocha huyp yupo jijini Mwanza na ameshaanza kutoa mapendekezo yake juu ya usajili wa mastaa wapya klabuni hapo ikiwemo usajili wa winga huyo msumbufu.
Pamba imeachana na karibia kikosi kizima kilichoipandisha daraja msimu uliopita huku wachache wanaohitajika wakipewa mikataba kimya kimya ya kusalia klabuni hapo ambapo wataungana na mastaa wapya kuunda jezi la kuutetea mkoa wa Mwanza katika ligi kuu nchini.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Mbali na Okuta kikosi hicho mpaka sasa kimeshawatambulisha Yona Amos,Samson Madeleke,Benny Nakibinde,Salehe Masoud,Ibrahim Abdallah,Justine Omary Billal na Frank Ng’amba.