Home Soka Dk.Mpango Aipamba Siku ya Wananchi

Dk.Mpango Aipamba Siku ya Wananchi

by Sports Leo
0 comments

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dk.Phillipo Mpango amehudhuria tamasha la siku ya mwananchi linalofanywa na klabu ya Yanga sc kwa ajili ya kutambulisha mastaa wapya kwa ajili ya msimu ujao.

Tamasha hilo limefanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam ikiwa ni mara ya sita kufanyika nchini na kuhudhuriwa na mashabiki lukuki wa klabu hiyo walioujaza uwanja huo mkubwa zaidi nchini.

Makamu wa Rais alikabidhiwa rasmi kadi ya uanachama wa klabu hiyo huku pia akikabidhiwa jezi ya klabu hiyo kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu.

banner

Katika Tamasha hilo Yanga sc ilicheza na making wa Kagame Cup timu ya Red Arrow kutoka Zambia na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 ambapo Ricky Banda alianza kuifunga Yanga sc kwa kichwa dakika ya 6 ya mchezo ambalo lilisawazishwa na Mudathir Yahaya kwa shuti kali kipindi cha pili huku Aziz ki akifunga kwa penati baada ya Nickson Kibabage kuangushwa eneo la hatari.

Tamasha hilo lilifana na kuwapa matumaini wananchi kuelekea mchezo wa August 8 dhidi ya Simba sc mchezo wa ngao ya jamii.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited