Klabu ya Simba Sc imeambulia sare ya 1-1 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Klabu ya Al Hilal Fc uliofanyika katika uwanja wa Kmc Complex uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam.
Simba sc ilitangulia kupata bao la kwanza dakika ya 26 ya mchezo likifungwa na Lionel Ateba baada ya shambulizi zuri lililoanzishwa na Ladack Chasambi.
Simba sc ilitawala mchezo huo huku ikionyesha kuanza kuelewana hasa eneo la kiungo na mabeki ambapo kocha Fadlu Davis ana kazi ya kutengeneza maelewano eneo la ushambuliaji.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kocha Florent Ibenge aliwaongoza vyema mastaa wa Al Hilal Fc ambao waliwakosa baadhi ya mastaa waliokwenda kujiunga na timu zao za Taifa na kufanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 86 ya mchezo.
Mpaka dakika 90 za mchezo huo zinamalizika matokeo yalibaki 1-1 huku baadhi ya mashabiki wa Simba sc wakionyesha kuridhika na kiwango cha timu na mastaa mmoja mmoja akiwemo Deborah Fernández.