Klabu ya Yanga sc imemtambulisha kocha Sead Ramovic kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo akichukua nafasi ya Miguel Gamondi ambaye ametimuliwa klabuni hapo kutokana na mwenendo mbaya wa kikosi hicho ndani na nje ya uwanja.
Ramovic amesaini mkataba wa mwaka mmoja klabuni hapo akitokea klabu ya Ts Galaxy ya nchini Afrika ya kusini ambapo atakua na jukumu la kuhakikisha klabu hiyo inatetea mataji yake ya ligi kuu ya soka ya Nbc sambamba na kombe la Shirikisho la Crdb pamoja na Ngao ya jamii.
Kocha huyo mwenye miaka 45 aliwahi kuzichezea klabu za Vfl Wolsfburg na Borrussia Monchengladbach zinazoshiriki ligi kuu ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga akicheza nafasi ya golikipa mpaka alipostaafu mwaka 2014 na kujikita kwenye kusomea ukocha.
Ajira yake ya kwanza kama kocha ilikua mwaka 2015 katika klabu ya Novi Pazar ya Serbia ambapo aliajiriwa kama kocha msaidizi ambapo alidumu mpaka mwaka 2020 alipojiunga kama kocha mkuu wa Ts Galaxy mpaka anajiunga na Yanga sc.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Msimu huu akiwa kocha wa Ts Galaxy katika michezo sita ya ligi kuu nchini humo hajapata ushindi wowote akipoteza mara mbili na kupata sare nne.
Kocha huyo anasifika kwa kupenda kutumia mfumo wa 4-2-3-1 ambapo mara kadhaa amefanikiwa kuwazuia vigogo wa soka nchini humo.