Home Soka Sita Watolewa kwa Mkopo Simba sc

Sita Watolewa kwa Mkopo Simba sc

by Dennis Msotwa
0 comments

Timu ya Simba sc imewatoa kwa mkopo nyota wake sita kwenda timu zingine ili wapate nafasi ya kucheza baada ya kukosa nafasi katika timu hiyo huku ikiachana na nyota saba ambao baadhi mikataba iliisha na wengine wametemwa kwa makubaliano maalumu ya pande mbili.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena mtendaji mkuu wa klabu hiyo Crescentius Magori alisema wachezaji waliotemwa baada ya mikataba kuisha ni Nicolaus Gyan,Emmanuel Okwi,Haruna Niyonzima,Deo Munishi,Zana Coulibary,James Kotei na Salim Mbonde huku Asante Kwasi  akiachwa baada ya pande mbili kukubaliana maana mkataba wake ulikua unaisha mwezi Novemba.

Pia timu hiyo iliyoweka kambi ya maandalizi ya mwanzoni mwa msimu nchini Afrika ya kusini imeamua kuwatoa kwa mkopo wachezaji sita ili wakaboreshe viwango vyao baada ya mwalimu kuona hawatopata nafasi ndani ya timu hiyo.Wachezaji hao ni Mohamed Ibrahim,Marcel Kaheza,Adam Salamba,Mohamed Rashid,Paul Bukaba na mchezaji aliyepandishwa kutoka timu ya vijana Abdul Athumani.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited