Klabu ya Tp Mazembe imeaga mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kufuatia kipigo cha 1-0 dhidi ya MC Alger kwenye mchezo wa raundi ya tano wa Kundi A uliofanyika nchini Algeria.
Mazembe licha ya kuwa wamebakisha mchezo mmoja ili kumaliza michezo ya makundi bado wanaendelea kusalia mkiani mwa msimamo wa Kundi hilo wakiwa na alama 2 baada ya mechi tano.
Kipigo cha Mazembe ambayo itakamilisha ratiba dhidi ya Al Hilal kinaiweka Yanga Sc ya Tanzania kwenye wakati mgumu zaidi wa kufuzu hatua ya robo fainali ambapo watatakiwa kushinda mechi zote mbili zilizosalia ili kufuzu tena kwa kuifunga MC Alger zaidi ya magoli matatu kwenye mchezo wa mwisho endapo watatoa sare na Al Hilal Omdurman.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Yanga sc itawavaa Al Hilal jumapili usiku ambapo matokeo ya ushindi katika mchezo huo yatatoa matumaini ya kufuzu.
Tp mazembe sasa wametolewa rasmi katika michuano hiyo msimu huu lakini bado wana nafasi ya kumaliza katika nafasi ya tatu ya msimamo wa kundi A endapo Yanga sc atapoteza michezo miwili na yeye kushinda mchezo ujao dhidi ya Al Hilal Omdurman.