Home Makala Singida Black Stars Yatema Bungo

Singida Black Stars Yatema Bungo

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Singida Black stars imetuma ombi rasmi katika klabu ya Gor Mahia ya nchini Kenya kutaka  kurejeshewa dau la usajili ambalo waliliweka kwenye akaunti zao kwa ajili ya manunuzi ya Ronney Onyango ambaye amegoma kujiunga na Black Stars licha ya makubaliano kati yao kufanyika.

Inaelezwa kuwa Gor Mahia walikubaliana na Singida kulipa kiasi cha dola 40,000 kwa ajili ya biashara hiyo ambapo Singida Black Stars  waliweka fedha kwa wakati kwa Gor Mahia lakini mchezaji amegoma kujiunga na timu hiyo.

banner

Mpaka sasa Staa huyo hajajiunga na timu hiyo ambayo imeweka kambi jijini Arusha kujiandaa na michuano ya ligi kuu nchini ambapo benchi jipya la ufundi la Klabu hiyo linapenyeza mbinu zake.

Katika msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini Singida Black stars ipo nafasi ya nne ya msimamo wa ligi kuu nchini ambayo imesimama mpaka machi mosi mwaka huu.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited