Mastaa saba waliokua na timu ya Simba sc nchini Afrika Kusini wanatarajiwa kurejea nchini kesho ili kujiunga na kambi ya timu ya taifa (Taifa stars) inayojiandaa na mchezo wa kufuzu michuano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani(Chan) dhidi ya Kenya.
Mastaa hao walioitwa kikosini na kaimu kocha mkuu Ettiene Ndayiragije akisaidiana na Seleman Matola ni Jonas Mkude,Ibrahim Ajib,Gadiel Michael,Hassan Dilunga,John Boko,Aishi Manula na Erasto Nyoni.
Kwa mujibu wa Afisa Mtendaji mkuu wa klabu hiyo wachezaji hao wameshindwa kusafiri leo kutokana na kukosekana kwa ndege ya Atcl ambayo kwa mujibu wa ratiba zake itasafiri kesho kuja nchini.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Simba sc imeweka kambi nchini Afrika Kusini kujiandaa na michuano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa na kurejea kwa wachezaji hao bila shaka kutaathiri programu ya mwalimu Patrick Asseums ambaye timu yake itavaana na Ud Songo ya Msumbiji katika hatua ya awali ya michuano ya kimataifa.