Klabu ya Wydad Athletic imemtambulisha rasmi kiungo mshambuliaji Stephan Aziz Ki iliyomsajili hivi karibuni kutoka klabu ya Yanga sc kwa mkataba wa miaka miwili.
Aziz Ki ametambulishwa klabuni hapo kupitia mitandao yake ya kijamii baada ya klabu hiyo kulipa takribani bilioni mbili ili kupata sahihi yake kutoka kwa klabu ya Yanga sc aliyokua na mkataba nayo wa mwaka mmoja.
Tayari punde tu baada ya kutambulishwa klabuni hapo nayo klabu ya Yanga sc ilichapisha maudhui rasmi ya kumuaga staa huyo aliyedumu klabuni hapo kwa misimu mitatu ya furaha.
Wakati akitambulishwa staa huyo aliambatana na mke wake Hamisa Mobeto sambamba na Meneja wake Zambro Traole ambao walishuhudia staa huyo akisaini mikataba hiyo na kutambulishwa rasmi.
Azizi Ki anatarajiwa kushiriki michuano ya klabu bingwa ya dunia mwezi ujao nchini Marekani ambapo jambo hilo ndilo limefanya usajili wake ukamilike mapema kabla ya dirisha la usajili nchini kufunguliwa.