Home Makala Ramovic Aibomoa Yanga Sc

Ramovic Aibomoa Yanga Sc

by Dennis Msotwa
0 comments
www.sportsleo.co.tz

Aliyekua kocha wa klabu ya Yanga sc Sead Ramovic ameibomoa klabu hiyo kwa kuwachukua watu wawili muhimu katika benchi la ufundi la klabu hiyo.

Ramovic amemuondoa mkurugenzi wa ufundi wa klabu hiyo Abdi Hamid Moallin ambaye anaondoka Yanga Sc na atajiunga na CR Belouizdad ya Algeria ya Kocha Sead Ramovic ambaye ndie aliyependekeza usajili wake.

Mbali na Moalin pia Mpho Maruping ambae alikuwa video Analyst wa Yanga sc ambaye sasa anajiunga na CR Belouizdad, Sead Ramovic, Abdi Hamid Moallin na Mpho wanaungana tena CR Belouizdad.

banner

Hata hivyo kuondoka kwa wataalamu hao kumetokana na kocha mpya wa Yanga sc Roman Folz kuamua kuja na safu yake mpya ya benchi la ufundi ambalo anaamini litafanya kazi yake kama anavyopenda.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited