Klabu ya Simba Sc imefanikiwa kufikia makubaliano na klabu ya Singida Black Stars juu ya usajili wa mshambuliaji Jonathan Sowah ambaye sasa atajiunga na klabu hiyo yenye makao yake makuu Msimbazi jijini Dar es Salaam.
Awali Singida Black Stars ilidai kuwa timu yeyote inayomhitaji mshambuliaji huyo inapaswa kulipa shilingi bilioni moja ili kuvunja mkataba wake uliosalia klabuni hapo.
Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo ya Singida Black Stars imesema kuwa dili hilo limekamilika kutokana na Rais wa heshima wa Singida Black Stars kuamua kumtoa mshambuliaji huyo kwa makubaliano maalumu na Rais wa heshima wa klabu ya Simba Sc Mohammed Dewji.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Baada ya makubaliano baina ya mabosi hao wa juu wa klabu hizo moja kwa moja klabu ya Simba Sc ilipewa ruhusa ya kuzungumza kuhusu maslahi binafsi ambapo walifikia makubaliano na sasa staa huyo moja kwa moja atajiunga na kambi ya Simba Sc moja kwa moja nchini Misri.