Bodi ya ligi kuu ya Tanzania bara (TPLB) imevifungia viwanja vya Mwadui complex,Manungu na Mabitini kutumika katika mechi za ligi kuu mpaka hapo vitakapofanyiwa ukarabati na kuthibitishwa na bodi hiyo kuwa vinafaa kutumika.
Akizungumza na waandishi wa habari afisa mtendaji mkuu wa bodi hiyo Michael Wambura amesema viwanja hivyo havirithishi kutumika katika michezo ya ligi kuu kutokana na kukosa ubora unaotakiwa yakiwemo majakwaa ya mashabiki.
Uwanja wa mabatini unatumiwa na klabu ya Jkt Tanzania kama uwanja wa nyumbani huku ule wa Manungu unatumiwa na Mtibwa Sugar na ule wa Mwadui Complex ulioko shinyanga unatumiwa na timu ya Mwadui Fc.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.