Home Soka Yanga Waikataa Nyekundu

Yanga Waikataa Nyekundu

by Sports Leo
0 comments

Timu ya soka ya Yanga sc wamekataa kutumia nembo ya mdhamini wa ligi kuu kampuni ya Vodacom baada ya nembo hiyo kuwa na rangi nyekundu kinyume na utamaduni wa klabu hiyo ambao ni mwiko kuweka rangi nyekundu katika jezi za klabu hiyo.

Fredrick Mwakalebela ambaye ni makamu mwenyekiti wa klabu hiyo amesisitiza kuwa klabu hiyo ina rangi tatu ambazo ni njano,kijani na nyeusi na Tff walilipitisha hilo hivyo wawaombe wadhamini waendane na matakwa yao.

“tulienda kupata dhamana na baraza la michezo la taifa na tuna rangi tatu,kijani,njano na nyeusi na Tff walilishalipitisha hilo kwahiyo tunashangaa wanapotuletea rangi ambayo hatukuipitisha sisi,Msimamo wetu ni kwamba wawaombe wadhamini tunawaheshimu,tunawapenda na tunawahitaji”.

banner

Kampuni ya vodacom imerudi kuidhamini ligi kuu ya Tanzania bara baada ya kutoongeza mkataba wa udhamini na kusababisha ligi hiyo kuchezwa bila mdhamini mkuu kwa msimu ulioisha.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited