Home Makala Boko Arejea Simba sc

Boko Arejea Simba sc

by Sports Leo
0 comments

Nahodha wa klabu ya Simba sc John Boko ameanza rasmi mazoezi baada ya kuwa nje kwa wiki kadhaa baada ya kupata jeraha katika mchezo wa kimataifa wa kufuzu klabu bingwa Afrika dhid ya Ud songo mchezo uliopigwa ugenini nchini Msumbiji.

Majeraha hayo yalimfanya Boko kukosa mechi ya marudiano iliyofanyika nchini na Simba kupoteza mechi hiyo kwa bao moja na kuwafanya kuyaaga mashindano hayo makubwa kwa ngazi ya vilabu barani Afrika.

Mshambuliaji huyo ameanza rasmi mazoezi hasa yale ya viungo chini ya kocha wa viungo Paul Gomez katika programu ya mazoezi ya timu hiyo inayofanyika katika viwanja vya gymkana jijini Dar es salaam.

banner

Hata hivyo ni ngumu mchezaji huyo kushiriki katika mchezo wa kesho dhidi ya Mtibwa sugar kutokana na kukosa utimamu wa mwili hasa baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited