Home Soka Kmc Yazinduka,Mtibwa Chali

Kmc Yazinduka,Mtibwa Chali

by Sports Leo
0 comments

Timu ya Kmc hatimaye imeonja ladha ya ushindi baada ya kuifunga Namungo Fc 1-0 katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa katika uwanja Chamazi complex jijini Dar es salaam.

Timu hiyo inayomilikiwa na manispaa ya kinondoni ilifanikiwa kuonyesha soka safi na kupata bao la kwanza kupitia kwa Hassan Kabunda aliyefunga dakika ya 38 bao ambalo lilidumu na kuifanya timu hiyo ipate ushindi wa kwanza baada ya kupoteza dhidi ya Azam fc na Coastal union.

Upande Mwingine Mtibwa sugar imekubali kipigo cha mabao matatu kutoka kwa Prisons katika uwanja wake wa nyumbani mjini Morogoro huku Biashara united nao wakipoteza kwa 1-0 dhidi ya Jkt Tanzania katika uwanja wake wa nyumbani mjini Musoma.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited