Timu ya Pyramids Fc imetua jijini Mwanza jana kwa kutumia ndege ya kukodi ambayo iliwatoa moja kwa moja kutoka nchini Misri mpaka jijini Mwanza kucheza mchezo wa kimataifa dhidi ya Yanga katika uwanja wa Ccm Kirumba.
Baada ya kutua kocha wa timu hiyo Sebastian Desabre alisema timu hiyo itajitahidi kuendana na mazingira ili kuweza kuibuka na ushindi katika mchezo huo japo mchezo hatutakuwa rahisi.
“Nawajua Yanga vizuri wakiwamo wachezaji wake kama yule Nahodha (Tshishimbi) na Balinya na ninawajua ni wazuri na mechi itakuwa ngumu ila tunataka ushindi” alisema Sebastien .
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Timu hiyo leo itafanya mazoezi katika uwanja wa Ccm kirumba ambao utatumika kwa ajili ya mchezo huo hapo kesho