Inadaiwa ni ngumu kumuchukua kocha wa Simba klabuni hapo kutokana na mahusiano na malengo aliyojiwekea na tajiri wa klabu hiyo bilionea Mohamed Dewji toka msimu uliopita.
Hivi karibuni zilisambaa tetesi za kochan huyo kuachana na klabuni hiyo baada ya kupata ofa katika klabu kadhaa ikiwemo As vita ya nchini Kongo huku klabu ya Nkana Fc ya nchini Zambia nayo ikimfikiria kwa ukaribu ili akachukua nafasi ya kocha mkuu baada ya kuachana na kocha wao.
“Lakini kwa sasa wanapaswa kujua bado nina mkataba na Simba ambao utamalizika Juni, mwakani na ukiangalia nina mikakati mikubwa ndani ya Simba ambayo tumekubaliana na uongozi wa timu kuona wapi tunakwenda na hilo kwangu ndiyo jambo kubwa,” alisema Aussems wakati akifanya mahojiano na vyombo vya habari.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kocha huyo amekua lulu barani Afrika baada ya kuisaidia Simba kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika kwa msimu ulioisha.