Home Soka 20 Yanga Kuifata Pyramids

20 Yanga Kuifata Pyramids

by Sports Leo
0 comments

Timu ya Yanga itaondoka nchini kesho kwenda nchini Misri kuifata Pyramids fc kucheza mchezo wa marudiano wa kutafuta nafasi ya kufuzu hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Katika kikosi hicho kilichotangazwa na Afisa habari wa klabu hiyo Hassan Bumbuli wamo makipa Farouk shikalo na Metacha Mnata huku mabeki wakiwa ni Juma Abdul,Ally Sonso,Ally Ally,Lamine Moro,Mharami Issa wakati viungo ni Feisal Salum,Papy Tshitshimbi,Mapinduzi Balama,Deus Kaseke,Abdulaziz Makame na Jaffar Mohamed.

Safu ya ushambuliaji ni Mrisho Ngasa,Patrick Sibomana,Sadney Urikhob,Juma Balinya na Issa Bigirimana huku Molinga na Mustapha selemani wakibaki kutokana na kukosa vibali wakati beki Kelvin Yondani anatumikia adhabu ya kadi nyekundu.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited