Home Soka Tambwe Awasubiri Yanga

Tambwe Awasubiri Yanga

by Sports Leo
0 comments

Mshambuliaji wa zamani wa Yanga Amissi Tambwe ameonyesha utayari wa kurejea Jangwani hata kwa mkataba wa muda mfupi

Tambwe anashikilia rekodi ya ufungaji mabao ligi ya Tanzania Bara kwa wachezaji wa nje akiwa amefunga mabao 73 tangu alipotua nchini msimu wa 2013/14

Msimu uliopita aliifungia Yanga mabao nane kwenye ligi hata hivyo hakupewa mkataba mpya

Alijiunga na klabu ya Fanja Fc ya Oman hata hivyo inaelezwa amevunja mkataba na kurejea kwao Burundi kutokana na matatizo ya kifamilia

Tambwe amesema bado anao uwezo wa kuzifumania nyavu na yuko tayari kurejea nchini kuitumikia Yanga hata kwa mkataba wa miezi sita

“Kama mabosi wa Yanga wakinihitaji niko tayari hata kwa mkataba wa miezi sita. Kikosi chao sio kibaya, tatizo ni safu ya ushambuliaji, mimi bado niko fit, uwezo wa kuwasaidia ninao” alisema

Kauli ya Tambwe imekuja wiki chache kabla ya kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili ambalo msimu huu litafunguliwa Disemba 15 badala ya Novemba 15 kama ilivyokuwa misimu ya nyuma

Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amependekeza maboresho katika kikosi chake, safu ya ushambuliaji ni miongoni mwa nafasi ambazo huenda zitaboreshwa

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited