Kocha Mkuu wa klabu ya Simba Patrick Aussems ameondoka leo asubuhi kuelekea nyumbani nchini Ubelgiji kwa kile kilichoelezwa kuwa ana matatizo ya kifamilia.
Habari kutoka klabuni hapo zinasema kuwa Aussems atakuwepo nchini humo kwa siku kadhaa na anategemewa kurejea kabla ya Novemba 24,ili kuiwahi mechi ya ligi kuu dhidi ya Ruvu shooting.
Kuondoka kwa kocha huyo mkuu kunamaanisha kwamba Kocha msaidizi Dennis Kitambi ndiye anayesimamia mazoezi kwa sasa akishirikiana na kocha wa viungo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.