Licha ya kufunga bao dhidi ya Redbull Salzburg straika wa timu ya Krc Genk Mbwana Samata ameshindwa kuiepusha timu hiyo na kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Salzburg mchezo uliochezwa nchini Ubeligiji.
Bao hilo alilofunga dakika ya 85 ni la tatu kwa staa huyo wa kitanzania katika michuano hiyo mikubwa barani ulaya huku mengine akifunga dhidi ya dhidi ya Liverpool na jingine aliifunga Salzburg katika mechi ya awali nchini Austria.
Genk tayari wametolewa katika michuano hiyo na wanasubiri mchezo wa kukamilisha ratiba dhidi ya Napoli baada ya kukubali vipigo katika michezo ya yote ya makundi waliyocheza mpaka sasa na kupoteza nafasi ya kushirika michuano ya europa baada ya kumaliza katika nafasi ya mwisho katika kundi.