Home Soka Watatu “Out” Stars

Watatu “Out” Stars

by Dennis Msotwa
0 comments

Wachezaji watatu wa Azam FC, viungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ pamoja na washambuliaji Shaban Chilunda na Iddi Seleman ‘Nado’ wameenguliwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania Bara kutokana na kuwa majeraha.

Kilimanjaro Stars ipo Kundi C pamoja na Kenya, Zanzibar na Djibout katika mashindano ya Chalenji yatakayofanyika jijini Kampala, Uganda kuanzia Jumamosi ya wiki hii.

Akizungumza jijini leo na waandishi wa khabari, Daktari wa Kilimanjaro Stars, Emil Urassa alisema wachezaji hao wameshindwa kupona majeraha yao kwa wakati hivyo benchi la ufundi limewaondoa katika hesabu yake. Urassa alisema.

banner

“Salum Abubakar aliripoti kambini, lakini alikuwa tayari na majeruhi aliyoyapata katika mchezo wa Azam na JKT Tanzania, pia Chilunda naye alionekana ana majeraha ambayo aliyapata katika mchezo wa mwisho wa timu yake. Iddi Seleman yeye aliumia katika mazoezi ya jana” alisema Dokta Urassa.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited