Mwenyekiti wa bodi ya Simba Mohammed Dewji ametangaza kujiuzuru nafasi yake katika bodi na kubaki kama mwekezaji.
Hii ni baada ya Simba kushindwa kuchukua Kombe la Mapinduzi kwa kufungwa na Mtibwa Sugar bao 1-0 na vijana hao kunyakua ubingwa katika uwanja wa Amani visiwani Zanzibar.
“Ni huruma Simba hawajaweza kushinda mchezo huu baada ya kuwalipa mishahara ya karibu bilioni 4 kwa mwaka ,hivyo najiuzuru kama mwenyekiti wa bodi na nitabaki kama mwekezaji Simba nguvu moja nitazingatia kukuza miundombinu na taaluma ya vijana “Alisema Mohammed Dewji.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.