Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Simba Sc Mohammed Dewji ametangaza kurejea kwenye nafasi ya uwenyekiti baada ya jana kutangaza kujiengua kufuatia kipigo cha bao 1-0 walichopigwa Simba kwenye fainali ya Mapinduzi Cup.
Aliomba radhi kutokana na akaunti zake kuibwa na nafasi hiyo kuchukuliwa kuposti maneno yale kupitia akaunti zake zote za mitandao ya kijamii.
Mohammed Dewji alisema “Kilichotokea jana sikukusudia ila tuko pamoja tunarudi kuendelea na ligi na tumejipanga pia nawapongeza Mtibwa Sugar kwa kuchukua kombe mimi ni SIMBA damu damu na nitabaki kuwa SIMBA”.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.