Home Makala Kichuya Anukia Yanga

Kichuya Anukia Yanga

by Sports Leo
0 comments

Mchezaji wa zamani wa Simba Sc Shiza Kichuya ambaye kwa sasa anakipiga kwenye klabu ya Pharco inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Misri aliyojiunga nayo mwaka jana baada ya kumalizana na Simba amekubali kusaini mkataba wa kucheza Yanga katika usajili wa dirisha dogo msimu huu wa ligi kuu Bara.

Kichuya alinunuliwa na Pharco kutoka Simba kwa dau la sh milioni 196 kabla ya kumtoa kwa mkopo ENPPI inayoshirki  ligi kuu kwa kumuongezea uzoefu zaidi.

Viongozi wa yanga wapo kwenye harakati za kukamilisha usajili wa mchezaji huyo ambaye ameomba kiasi cha milioni 30 kwa mkopo wa miezi sita pekee ikiwa kichuya mwenyewe anachelewesha kutokana na kutopunguza dau hilo kwani haliendani na muda anaotaka.

banner

Uongozi umehaidi kumsainisha mchezaji huyo kwa dau alilotaka kama ataichezea Yanga kwa muda wa miaka miwili huku mkurugenzi wa uwekezaji wa kampuni ya GSM Hersi Said akisema”kila kitu kuhusiana na usajili kipo kwenye benchi la ufundi ,sisi ni kampuni tunawezesha katika kutoa pesa”.

 

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited