Baada ya kukaribia kukamilisha usajili kwenda klabu ya Aston Villa inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza imesadika kuwa mauzo ya mchezaji huyo yataifaidisha klabu ya Simba ambayo aliichezea staa huyo kabla ya kutimkia Tp Mazembe ya nchini Drc.
Samatta aliuzwa na Simba kwenda klabu hiyo ambayo nayo ilimuuza kwenda Krc Genk mwaka 2016 ambapo katika mauzo hayo klabu ya Simba ilipata mgao wa dola 50000 japo inasemekana ilikua ilipate dola 100000 kulingana na mkataba.
Hivi sasa staa huyo yupo nchini Uingereza akikamilisha taratibu za uhamisho na endapo usajili huo ukikamilika kwa mujibu wa Fifa kila klabu aliyopitia staa huyo inatakiwa ipate mgawo wa asilimia kwa mujibu wa kanuni za Fifa,hivyo klabu hiyo inakadiriwa itaingiza takribani bilioni 1.2 endapo usajili wa paundi milioni 9 ukikamilika.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.