Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesepa na pointi tatu muhimu kwa mara ya kwanza kwa ushindi wa mabao 3-1 mbele ya Singida United katika uwanja wa Namfua.
Molinga alipachika bao la kwanza dakika ya 12 na kipindi cha pili waliongeza juhudi na kufunga bao la pili kupitia kwa Haruna Niyonzima dakika ya 57 akimalizia pasi ya Morison.
Wakati mabeki wa Singida United wakijitahidi kuokoa mpira ulio ndani ya 18 mchezaji wa Yanga Yikpe aliongeza bao la tatu dakika ya 77 huku Singida United wakijipatia bao la kufuta machozi dakika ya 82 kupitia Six Mwakasege. .
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Luc Eymael alisema kuwa walijipanga kupata ushindi na hivyo ahadi imetimia kwa mashabiki wa Yanga.’8