Liverpool imebaki nafasi ya kwanza ikiwa imewapiga West Ham United mabao 2-0 katika michuano ya ligi kuu England siku ya jana uwanja wa London Stadium wakisimamiwa na refa kutoka England Jonathan Moss.
Mshambuliaji wa liverpool Mohamed Salah alianza kuipatia bao la kwanza timu yake kupitia penalti aliyopewa na Jonathan ikiwa ni adhabu ya Westham dakika ya 35 huku bao la pili lilipatikana dakika ya 52 kupitia Alex Oxlade Chamberlain.
Wachezaji wawili wa WestHam ndio waliopokea kadi za njano katika mchezo wa jana ambao ni Issa Diop dakika ya 34 na dakika ya 43 alipokea Mark Noble.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
West Ham United inabaki kushika mkia nafasi ya 17 na pointi 23 ikiwa imecheza mechi 24 huku Liverpool inabaki nafasi ya 1 ikiwa imecheza mechi 24 na pointi 70 zenye kuleta furaha kwa mashabiki wake.